-->

Rapper Soulja Boy karudi kwenye game, asainiwa na kampuni hii kubwa

GUSA HAPA CHINI KUPLAY VIDEO

Rapper Soulja Boy karudi kwenye game, asainiwa na kampuni hii kubwa

Rapper Soulja Boy ametoa ahadi ya kurudi kwenye game ya muziki wa Hip Hop baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma na wengi kuhoji kuwa huenda akawa amepotea kwenye game kutokana na ushindani mkubwa uliopo nchini Marekani.

Soulja Boy amewafurahisha wengi baada ya kuja na good news kuwa yuko tayari kurudi kwenye mstari na kutoa ngoma kila mara na kufanya kazi kwa bidii na hii ni baada ya kusajiliwa rasmi na kampuni ya muziki ya Entertainment One Music iliyopo huko Marekani.
Mkali huyo wa rap aliwahi kuhit na ngoma ya ‘Kiss Me Through The Phone’ mwaka 2009 na ametoa taarifa hizo kupitia mtandao wa twitter, kampuni hiyo ya Entertainment One Music imewahi kufanya kazi na wakongwe kibao akiwemo Snoop Dogg, The Game,Tupac, Marehemu Michael Jackson na wengine wengi.

Soulja Boy ameandika “Ni rasmi kuwa nimesajaliwa na Entertainment One Music asanteni mashabiki wangu, naahidi kuachia ngoma mpya na kufanya kazi kwa bidii”

Share :
Facebook Twitter Google+

 
Back To Top