Leo November 23, 2018 Tunae Mke wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Agrey Mwanri katika Exclusive Interview na AyoTV na millardayo.com ambapo ametueleza mambo mengi ikiwemo maisha ya Mumewe akiwa nyumbani na jinsi ambavyo yeye anamchukulia.
Mke wa RC Mwanri ambae jina lake ni Grace Mwanri nimemnukuu akisema “Watu wanaomfahamu wa karibu sio mkali wakusema ni kumuogopa kiasi kile, ukiona ameongea vile jua amekereka au ameudhiwa, anataka watu wafanye walichoagizwa si na Serikali tu! ila hata na Mungu”
“Katika Familia yetu ni mtu mcheshi sana tunatamani kuwa nae, sababu tukiwa nae tunatia stori, tunaongea tunafurahi huwezi kuta tumekasirikiana si Mimi wala kwa Watoto” -Grace Mwanri
“Akiwa kwenye msiba akitoa salamu au akizungumza watu huwa wanajisahau wapo msibani wanaanza kushangilia na kuanza kupiga makofi hicho ni kitu Mungu ameweka ndani yake” -Grace Mwanri

