UKIHADITHIWA tu na mtu yeyote unaweza kusema ni hadithi ya kutungwa, lakini ukweli ni kwamba kuna watu huko kwenye visiwa vya Papua New Guinea ambavyo vimezungukwa na bahari inayoitwa Bismarck Sea wanakula binadamu wenzao.
Nchi hiyo yenye watu wapatao milioni 7.3 ina makabila mengi yanayotofautiana mila. Tena basi mengine yana mila mbaya na za kutisha na wanakiuka haki za binadamu kwa kiasi kikubwa. Katika mapori wanaoishi watu hao ni jambo la kawaida mtu ‘akionwa’ na wazee wa kimila kwamba...
